KAIRUKI AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KUUNGA MKONO UJENZI WA KILIMA KWA YUSUFU


Mbunge wa Jimbo la Kibamba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amekabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa Kilima kwa Yusufu, hatua inayolenga kuharakisha utekelezaji wa mradi huo na kuimarisha maendeleo ya jamii kupitia ushirikiano kati ya Serikali na wananchi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kairuki amewapongeza viongozi na wananchi wa eneo hilo kwa kujitolea kushiriki katika shughuli za maendeleo, akieleza kuwa mafanikio ya miradi ya kijamii yanategemea mshikamano, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika hatua zote za utekelezaji.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha miundombinu inayojengwa inalindwa na kutunzwa ili iweze kuwanufaisha wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wao, viongozi wa Kilima kwa Yusufu wamemshukuru Kairuki kwa msaada huo wa mifuko 100 ya saruji, wakisema utachochea kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuboresha huduma kwa wananchi. 

Pia wameahidi kuitumia saruji hiyo kwa ufanisi na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post