Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na Mhe. Yomna Elbahar, Naibu Waziri wa Utalii na Mambokale aliyeongozana na Dkt. Nader El Niblawi, Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala zaidi ya 2,300 wa Utalii nchini Misri, wamehitimisha leo Juni 9, 2026, kongamano la Utalii, Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Misri.
Mwaka jana 2025 jumla ya watalii 6,000 kutoka Tanzania walitembelea Misri huku Tanzania ikipokea takribani watalii 8,000 kutoka Misri.
Nchi hizi mbili zina uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu tangu enzi za urafiki wa Mwalimu Julius Nyerere na Rais Gamal Abdul Nasser; Tanzania ndio chanzo kimojawapo cha Mto Nile; uhai muhimu wa Taifa la Misri, kampuni za Misri za Arab Contractors na Elsewerdy Electric ndizo zilizokubali na hatimaye kukamilisha Bwawa la Umeme wa Maji la Julius Nyerere nchini Tanzania.
Misri inapokea zaidi ya watalii milioni 16 kutoka mataifa mbalimbali ambapo pia imeanzisha safari za Egypt Air kuja Tanzania mara tatu kwa wiki.
Viongozi hao wamekubaliana, kupitia ofisi zao, na sekta binafsi ya pande zote mbili, kuongeza biashara, uwekezaji na hususani idadi ya watalii.
