MAFUNZO YA UMOJA WA WABUNGE VIJANA TANZANIA DODOMA


Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Vijana Tanzania (TYPC) Mhe. Zainabu Katimba akizungumza na kuongoza mkutano wa Mafunzo ya Umoja wa Wabunge Vijana Tanzania (TYPC) Bungeni Jijini Dodoma Leo Tarehe 16 June 2026.

Mgeni Rasmi ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka.

Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo kuhusu uongozi, utungaji wa sheria, usimamizi wa rasilimali za umma na namna bora ya kuwakilisha maslahi ya vijana katika mchakato wa maendeleo ya taifa.

Mafunzo haya pia yameweka mkazo katika kuimarisha ushiriki wa vijana katika maamuzi ya kisera na kisiasa, huku yakitoa fursa kwa wabunge vijana kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii, hususan vijana.

 Washiriki wameeleza kuwa mafunzo hayo yataongeza ufanisi wao katika kutekeleza majukumu ya uwakilishi, ushauri na usimamizi kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post