BWANKU AITUMIA JUMAMOSI HII KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KUPITIA MKUTANO- KATA YA KASHARU


Leo Jumamosi Juni 06, 2026 Afisa Tarafa ya Katerero, Bwanku M Bwanku iliyopo Bukoba mkoani Kagera ameongozana na Diwani wa Kata ya Kasharu Mhe. Naswiru Musa, Mtendaji wa Kata, Dickson Adrian, Polisi Kata Afande Alan 

Nkooko na Uongozi wa Kijiji cha Kabajuga ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Selemani Musa na Mtendaji wa Kijiji Bi. Shani Kazinja kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji cha Kabajuga na viongozi kuzitolea ufafanuzi.

Mkutano huo na wananchi wa Kijiji cha Kabajuga ulilenga kutatua mgogoro wa ardhi Kijijini hapo pamoja na kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama ili kuhakikisha wananchi wanakua salama wao na mali zao.

Wananchi walipata nafasi ya kueleza masuala mbalimbali kuhusu suala la ardhi ya kijiji inayodaiwa kuchukuliwa pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya kijiji ili kudhibiti wizi na uhalifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post