RC LINDI AKABIDHI VITENDEA KAZI VYA USAFIRI LINDI KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA


Mkuu wa Mkoa wa Lindi  Mhe. Zainab  Telack amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa  TANESCO Mkoani humo ili kuongeza kasi na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja.

Mkuu huyo wa Wilaya amekabidhi vitendea kazi hivyo  April 15,  2026 yakiwemo magari 4, bajaji 7 na pikipiki 10 ambavyo vitapelekwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ili kuwafikia wananchi bila kujali jiografia ya eneo husika.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati na kwa ufanisi.

‘’ Vitendea kazi hivi vitakuwa chachu ya kumfikia mteja kwa haraka, hii ni dhamira ya Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme lakini wanafikiwa kwa haraka wanapopata changamoto za umeme’’alisema Mhe. Telack.

Katika hafla hiyo, Mkuu  huyo wa Mkoa pia alikabidhi majiko ya  umeme yanayotumia  umeme kidogo kwa baadhi ya wateja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya Serikali ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. 

Katika kuongeza uelewa kwa wananchi Mhe. Telack pia  alikabidhi jiko kwa mmoja wa watumishi wa TANESCO Mkoani Lindi  ili kuwa balozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii inayomzunguka.

"Kwa niaba ya watumishi wa TANESCO, nakukabidhi jiko hili ili utumie na  kuhahamasisha  wananchi kwa vitendo juu ya  umuhimu wa kutumia majiko haya ya umeme ambayo ni salama na nafuu,’’alisisitiza Mhe. Telack

Naye  Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi,  Theodory Hall, alikabidhi majiko sanifu yanayotumia umeme kidogo kupikia  kwa Mkuu wa Mkoa  Mhe.Zainab Telack na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Zuwena Omary  ishara ya kuunga mkono jitihada na kampeni ya Kinara wa Nishati safi  ya kupikia ambaye ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt  Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

Previous Post Next Post