Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenan Kihongosi leo Machi 4,2025 amewasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yake katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa.
Ziara hiyo itahusisha Mkoa wa Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Geita, katika ziara hiyo Kihongozi anatarajiwa kushiriki shughuli mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kutembelea mashina mikutano ya hadhara ili kuzungumza na wananchi.
Katika Mkoa wa Shinyanga amepokelewa katika Kata ya Isaka Jimbo la Msalala wilayani Kahama na anatarajiwa kukagua miradi miwili ya maendeleo ambao ni Mradi wa Bandari Kavu ya Msalala na ujenzi stendi ya Kahama Mjini.
Akitoa salamu baada ya Kihongosi alitoa neno na kueleza kuwa ziara hiyo imelenga kuangalia uhai wa chama cha CCM kwa kutembelea mashina, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Katika hatua nyingine Kihongosi ametoa mwito kwa wananchi kuwa kila mmoja anawajibu wa kulinda amani na utulivu uliopo kwani wamekusanyika mahali hapo kwa sababu ya amani na utulivu uliopo nchini.
“Tumekusanyika kwa sababu nchi yetu ina amani na utulivu tunaona abaadhi ya maeneo duniani kuna vurugu kubwa ambazo zinaendelea watoto na kina mama wanafariki nchi zao hazina utulivu lakini ndani ga taifa letu Mungu ametujaalia upendo,” amesema Kihongosi.
Pia alifikisha salamu za Mwenyekiti wa Chama Taifa , Dk Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa Chama , Balozi Dk Asha Rose Migiro ambaye alisema atatembelea mabalozi wa mkoa huo.
