DMF WAZINDUA WODI YA WATOTO, JANABI AMWAKILISHA TEDROS

 


Jengo la kisasa lenye viwango vya Kimataifa la kuhudumia Watoto njiti limezinduliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Mohamed Janabi ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Jengo hilo limejengwa na Taasisi ya Doris Mollel (@dorismollelfoundation) chini ya Mkurugenzi Mkuu wake Doris Mollel (@dorismollel) kwa kushirikiana na Wadau Maendeleo wakiwemo Taasisi ya Keep A Child Alive ya Msanii maarufu wa Marekani Alicia Keys, Jhpiego na DAMAC Foundation na Marafiki wa Doris Mollel Foundation.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Janabi amesema Tanzania imeendelea kupiga hatua katika kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano, vikishuka kutoka 81 hadi 68 kwa kila Watoto 1,000 wanaozaliwa hai kati ya mwaka 2015 na 2022 akisema mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa sekta ya afya akiwemo Doris Mollel.

Post a Comment

Previous Post Next Post