TANZANIA YAPEWA MAUA KULINDA HAKI ZA BINADAMU


Wakati mwenendo wa hali ya haki za binadamu  baadhi ya mataifa duniani ukiwa mbaya; Tanzania imemwagiwa sifa kuwa na mwenendo mzuri wa kushughulikia haki za binadamu.

Sifa hizo kwa Tanzania zilitolewa na Kamishina Mkuu wa HRC, Volker Turk katika Hotuba yake ya Ufunguzi kuhusu Hali ya Haki za Binadamu Duniani, wakati wa Kikao cha 61 cha baraza hilo, kilichofanyika Geneva, Uswisi.

Katika hotuba hiyo  iliyosheheni rekodi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu duniani ikiwemo Marekani, Kamishna Turk alisema baraza hilo linatambua na kuthamini hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania za kuanzisha Tume ya  Uchunguzi kufuatia  vurugu  zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu  wa Oktoba, 2025 

Hatua hiyo ya Tanzania kutajwa kwa sifa hizo nzuri na Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Duniani; inaendeleza rekodi na taswira nzuri ya kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Tayari wafuatiliaji wa masuala ya haki za binadamu duniani wameshauri matokeo ya ripoti  hiyo ya Tume  yazingatie misingi na  juhudi za kutekeleza haki za binadamu, mambo ambayo yanatarajiwa kuzingatiwa kutokana na uhuru na weledi wa wajumbe wake wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande.

Tanzania ikisifiwa, mwenendo wa haki za binadamu umetajwa kuwa mbaya Marekani, ambako operesheni dhidi ya wahamiaji haramu imetajwa kuendeshwa kwa kukiuka misingi ya haki za binadamu. 

Iran, imechomoza kuwa na hali mbaya ya haki za binadamu huku ikitumiwa kukandamiza waandamanaji na kuwahukumu kifo wakiwemo watoto.

Post a Comment

Previous Post Next Post