Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameshiriki katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Mwigulu Nchemba alipofika jimbo la Bumbuli Wilaya ya Lushoto mkoa wa Tanga eneo la Soni kwa Mkutano wa hadhara na wanachi.
Aidha akizungumza na kutoa salam za Wizara ya Maji ameeleza kuwa Serikali inakwenda kujenga Mradi wa gharama ya Bilioni 16 ili kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya uhakika ya Maji Soni na tayari kazi ya usanifu imekamilika.
Waziri Mkuu Mhe Dkt Mwigulu Nchemba anaendelea na ziara yake mkoani Tanga akihitimisha leo kazi katika wilaya ya Lushoto.
