Nchi za Tanzania na Uganda zitaendelea kushirikiana katika uhifadhi wa malikale zilizoko katika mataifa hayo.
Hayo yamejadiliwa katika kikao cha pamoja kati ya Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii alipokutana na pacha wake, Katibu Mkuu wa Utalii, Wanyamapori na Malikale wa Uganda, Mama Doreen Katusiime.
Kikao hicho kilichohusisha pia wataalam wa pande zote mbili kimefanyika pembeni ya Mkutano wa 47 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO unaoendelea jijini Paris, Ufaransa.
Tanzania na Uganda pamoja na mambo mengine zina maeneo yanayofanana ya malikale ikiwemo michoro ya kale ya miamba hasa eneo linalozunguka ukanda wa Ziwa Viktoria.