Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa Wilayani Urambo katika ziara ya kikazi ya kimkakati ya kutembelea, kukagua na kujionea maendeleo ya Kazi ya Utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji28 kwa Miji ya Urambo, Kaliua na Sikonge.
Akiwa maeneo ya matukio Waziri Aweso ameshuhudia ulazaji wa bomba la milimita 300 kijiji cha Kalemela B, Urambo.
Aidha, amekagua ujenzi wa matenki mawili katika kijiji cha Kalemela B, Urambo lenye ujazo wa Lita 2,000,000 na tenki la Misheni, Sikonge lenye ujazo wa Lita 1,000,000.
Mradi huu uliokaguliwa unahusisha kazi za Ulazaji wa mabomba makuu zaidi kilomita 190, ujenzi wa matenki 5 yenye ujazo wa jumla ya Lita 8,000,000 na mabomba ya usambazaji zaidi ya kilomita 100. Mradi umeanza kutekelezwa tarehe 11 Aprili 2023 na unategemewa kukamilika mwezi Oktoba 2025.
Gharama ya mradi kwa Miji yote mitatu ni zaidi ya shilingi bilioni 143 na utahudumia wananchi zaidi 490,000.
