MAMENEJA WA HOTELI ZANZIBAR WAKUTANA NA TCRA MJINI MAGHARIBI


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ofisi ya Zanzibar ikiongozwa na Meneja Bi. Esuvatie-Aisa Masinga  imeendesha mkutano pamoja na mameneja wa hoteli za Mkoa wa Mjini Magharibi, ukumbi ni wa ZSSF Kariakoo tarehe 18 Julai, 2025. 

Mkutano huo umelenga kujadili na kuratibu kwa pamoja namna bora ya kuandaa mazingira rafiki ya mawasiliano hususan katika maeneo ya hoteli za Mkoa wa Mjini Magharibi, pamoja na utaratibu wa kuomba na kupata leseni za Mamlaka kwa utumiaji wa redio za mawasiliano (VHF/UHF).

Mameneja na maofisa kutoka ofisi ya zanzibar , vitengo vya Masuala ya Wateja na Watumiaji, Usimamizi wa Masafa,  Leseni pamoja na Ufuatiliaji na Utekelezaji kutoka TCRA Makao Makuu wametoa mawasilisho mbalimbali pamoja na kupokea na kujibu maswali ya wadau hao.

TCRA hutumia dhana ya usimamizi kwa mashauriano (regulation by consultation)  na hukutana mara kwa mara na wadau wa sekta wakiwemo watoa huduma, ili kuhakikisha mustakabali bora wa ukuaji wa sekta ya mawasiliano pamoja na matumizi chanya ya fursa zinazoletwa na ukuaji wa teknolojia kwa maendeleo ya uchumi wa kidijiti na wa buluu. 

Pia, tunakukumbusha kutembelea tovuti ya TCRA (www.tcra.go.tz), au kupitia kiunganisho https://bit.ly/44tXbii ilikupitia ripoti  ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano (Aprili - Juni 2025).

Post a Comment

Previous Post Next Post