Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Charles Mwanziva amehitimisha kwa kishindo ziara ya kikazi Kata kwa Kata katika kata zote za Jimbo la Mchinga- Lindi Manispaa ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Wilaya nzima ya Lindi katika majimbo matatu ya Lindi Mjini, Mchinga na Mtama.
Wanachi wa Manispaa ya Lindi jimbo la Mchinga wamemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa ya maendeleo wanayonufaika nayo ambapo Ziara hii ya kimkakati imewezesha kuweka Mawe ya msingi na kuzindua miradi kwenye Sekta ya Afya, Elimu, Maji na Miundombinu.
Pia, Ziara ya Mkuu wa Wilaya imetembelea na kukagua safari ya maendeleo na muendelezo wa utoaji wa huduma za Ugani, Afya, Elimu- sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Ziara hii kwa umuhimu mkubwa imekua ni fursa nzuri kwa wananchi kutoa na kusikilizwa na kupata utatuzi wa changamoto zao kwa kuwafikia kwa wingi katika maeneo yao kwa kufanya mikutano ya hadhara na vikao kazi na Watumishi na wananchi.