KAWAIDA: VIONGOZI BORA WANATOKANA NA CCM


Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Ali Kawaida amesema viongozi bora ambao wataongoza Wananchi vizuri na kuleta maendeleo wanatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) pekee.

Kawaida amesema hayo leo tarehe 10 Aprili 2025 akizungumza na Umoja wa Madereva wa Bajaji mkoani Iringa baada ya kuanza ziara yake ya siku mbili akizungumza na makundi mbalimbali ya vijana, kufungua miradi ya vitega uchumi ya UVCCM mkoani hapo pamoja na kushiriki kongamano litakalo angazia Ushiriki wa Vijana katika Uchaguzi Mkuu.

Kawaida amesema kauli hiyo kuhusu kiongozi bora ilitolewa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere ila bado inaishi kutokana na viongozi bora ambao wanapikwa na CCM na kuwaomba kumrudisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu kwa kumpigia kura za kishindo.

"Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ndugu zangu, muda ukifika watakuja watu wengi ila Chama pekee ambacho chenye viongozi bora ni CCM," amesema Kawaida

Akizungumzia ushiriki wa Ushiriki wa Uchaguzi Mkuu, Kawaida amesema Chama cha Mapinduzi kipo tayari kwa uchaguzi huo na hakuna wa kuuzuia.

"Kuna watu wanasema wanahitaji mabadiliko ya sheria ndio washiriki uchaguzi, binafsi nawashangaa sana, serikali kwa mara ya kwanza wametengeneza sheria na kufanya marekebisho makubwa ya sheria za uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa uhuru na haki, tume ya uchaguzi imebadilishwa kutoka tume ya uchaguzi kuwa tume huru ya uchaguzi, kama wameona hawawezi kushindana na wagombea wa CCM wasitafute sababu waseme ukweli," amesema Kawaida

Awali Kawaida alifungua kitega uchumi cha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani Iringa zikiwa fremu 11 na eneo la biashara ambalo amepewa Mwekezaji kujenga jengo la biashara ili liweze kuzalisha mapato na kutoa ajira hivyo amewataka kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili kujiingizia kipato.

Post a Comment

Previous Post Next Post