Waziri wa nchi ofisi ya Rais (mipango na uwekezaji ) mhe. Prof Kitila mkumbo amesema amefanikiwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya mendeleo katika mkoa wa Manyara ipatayo kumi na moja (11) kama sampuli tu yenye thamani zaidi ya bilioni 11
Ameyasema hayo hii leo Jumamosi ya Januari 4, 2025 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Gallapo kilichopo halmashauri ya wilaya ya babati vijijini wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Manyara iliyolenga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo mkoani humo iliyoanza Januari 2, 2025 na kukamilika hii leo Januari 4, 2025
Prof Kitila amehitimisha ziara yake hii leo kwa kutembelea wilaya ya babati katika halmashauri mbili(2) tofauti ambazo ni halmashauri ya wilaya ya babati vijijini na halmashauri ya mji wa babati
Ambapo katika halmashauri ya wilaya ya babati vijijini amezindua kituo cha afya cha bashnet kilichogharimu zaidi ya shilingi millioni mia sita(632,221,000),pia amezindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya billioni mbili na katika halmashauri ya mji wa babati amezindua kituo cha afya Sigino kilichogharimu shilingi millioni mia nne(400,000,000) na kuhitimisha kwa kuzindua jengo la watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda(premature) jengo hilo lililogharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/=