Waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri wameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea, kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maji Geita.
Wameufikia Mradi wa Maji wa Bwanga wa thamani ya Bilion 1.6, na kuridhika na kazi aliofanya Mkandarasi Otonde Company Ltd na kwa hakika kazi nzuri imefanyika, baadhi ya Vijiji tayari vinapata Maji.
Waziri Aweso amesema Mradi huu muhimu katika eneo hili lililokua na changamoto kubwa ya Maji na ameuwekea jiwe la msingi na kuelekeza ukamilike ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuzinduliwa.