Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Songea mkoa wa Ruvuma waliojitokeza kwa wingi leo terehe 28 Septemba 2024 uwanja wa Majimaji.
Akizungumzia Sekta ya Maji amesema kazi inaendelea na aliweza kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji Mtyangimbole Madaba na akiwa njiani kuelekea Tunduru kupitia Namtumbo yapo maeneo yaliokua na changamoto ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa mkandarasi Mchomoro kusuasua na wananchi wa eneo la Kilimasera waliohitaji Maji na kuipongeza Wizara kwa kufanyia kazi kwa haraka katika maeneo haya yote na kumshukuru Waziri wa Maji kwa niaba ya watendaji wote wa sekta.
Aidha, Baada ya Maelekezo haya Waziri wa Majie Mheshimiwa Jumaa Aweso ameyateleza kwa haraka ikiwa ni pamoja na kazi ya uchimbaji kisima kuendelea Kilimasera na upande mradi mkubwa wa Maji wa Mchomoro kuhakikisha vifaa vyote vinafika eneo la mradi na mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana kazi ikamilike haraka.