MHE UMMY ATOA SIMU 27 CCM WILAYA YA TANGA.

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 14/09/2024 amekabidhi simu 27 zenye thamani ya shilingi milioni 9 kwa  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga ndg Meja Mstaafu Hamisi  Mkoba, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Tanga na Sekretariati ya Wilaya.

Simu hizo ambazo Mhe Ummy amezitoa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa tarehe 17/08/2024 mbele ya Mhe Hemed Abdulah, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga alipofanya Ziara yake Wilaya ya Tanga.

Simu hizo 27 ambazo zimetolewa na Mhe Ummy ni kwa ajili ya kuchochea kazi ya usajili wa wanaCCM kieletronic na zitasambazwa katika kata zote 27  za Tanga Mjini. Awali, mwaka 2023 Mhe Ummy alitoa simu 4 na hivyo sasa kufanya jumla ya simu 31 ambazo zimetolewa na Mhe Ummy kwenye Chama.

Post a Comment

Previous Post Next Post