Mkurugenzi wa huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea leo leo Septemba 5, 2024 amekutana na Taasisi ya The Healthier kidney Foundation ambao ni waandaaji wa Figo Marathon.
Katika mazungumzo yao Dkt. Nyembea ameipongeza Taasisi The Healthier kidney Foundation kwa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujenga taifa lenye afya imara na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyo ambukiza hususani Figo.
Wizara inaendelea kushirikiana na wadau ili kubadili mitindo ya maisha hatarishi na kuwa na jamii yenye ustawi bora wa afya kwa kufanya mazoezi yaliyo bora.
Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Jenipher Mambo pamoja na Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi hiyo Maulid Juma wamefanikiwa kuzindua sare rasmi za Figo Marathon kwa Msimu wa tatu zitakazofanyika Septemba 22, 2024. Jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
Taasisi The Healthier kidney Foundation Kupitia Mbio za Figo Marathon 2024 imeadhimia, kupeleka sehemu ya Mapato hayo kuboresha huduma za Afya nchini na kusaidia matibabu ya watoto wapatao 50 wenye changamoto za magonjwa ya Figo .