AWESO AWASHA MOTO JIJINI MWANZA,ASEMA KAZI YA UJENZI MRADI BUHONGWA IFANYIKE USIKU NA MCHANA


Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso Leo tarehe 08/09/2024 ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kuboresha wingi wa maji kata za Buhongwa na Lwanhima na kuelekeza wananchi wa maeneo haya kupata Maji haraka ndani ya wiki hii.

Mradi huu una gharama ya Tshs. Milioni 864.816. Mradi huu utanufaisha wakazi wa mitaa ya Sahwa ya chini, Sahwa ya juu, Buhongwa mashariki, Buhongwa magharibi, Buhongwa centre na Maliza. 

Kazi kubwa ya utekelezaji wa Mradi huu imefanyika chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA Bi. Nelly Msuya hivyo kuagiza kazi iliobaki ikamilike haraka.

Wakati wa ziara hiyo Mhe Waziri ametoa maelekezo makali na kueleza namna gani wananchi wa maeneo hayo wamekua wakiteseka na kuhangaika kupata huduma ya maji na kusisitiza kuwa kazi hiyo ifanyike usiku na mchana na kwamba usiku wa leo yeye binafsi atakwenda kuangalia tena utekelezaji wa kazi hiyo usiku wa leo kuona kile alichaogiza mchana kinafanyika.

Post a Comment

Previous Post Next Post