KUJITUMA KWENU KUTAJENGA DAWASA ILIYO BORA"-AWESO


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo tar. 04 Julai 2024 amefika Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar Es Salaam kutembelea na kukagua Mradi Mkubwa wa Maji katika Miundombinu ya Tenki la Maji lita mil.15.

Waziri Aweso anaendelea na ziara ya kikazi mkoa wa Dar Es Salaam.

Katika hatua nyingine Mhe Aweso amekutana na Watumishi wa mkoa wa DAWASA - Kigamboni ambapo  amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa bidii na kudumisha umoja ili kuleta maendeleo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mhe. Aweso pia ameelekeza uongozi wa DAWASA kuboresha huduma ya maji Kigamboni ili kila mwananchi anufaike na huduma ya Maji.

Post a Comment

Previous Post Next Post