TANZANIA NA MAREKANI KUSHIRIKIANA ZAIDI KATIKA SEKTA YA AFYA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu Leo Mei 28, 2024, akiwa katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini Dar es Salaam amefanya Mazungumzo na Wageni kutoka baraza la Congress Marekani (The United States Congressional Staff Delegation).


Msafara huo ambao umeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CDC Ofisi ya Washington Jeff Reczek Wamekutana na Dkt. Jingu na kujadili ushirikiano wa Serikali ya Marekeni na Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma za Afya nchini. 


Dkt. Jingu pia ametumia fursa ya ugeni huo kutuma salamu shukurani kwa serikali ya Marekani kwa mchango wao katika kuiwezesha Tanzania kutekeleza afua mbalimbali za huduma za afya na pia kuisadia Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama Murbag na Covid-19


Kwa kipindi chote watakachokuwepo nchini Wageni hao pia watapata fursa ya kutembelea Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kushuhudia hafla ya makabidhiano ya Maabara ya Hospitali ya Kanda Bungando na kutembelea pia Kituo cha Operesheni ya Dharura Mwanza (Emergency Operation Center) ili kujifunza na kujionea utendaji kazi wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post