LUSANGA BINGWA MWANAFA CUP, SCOUT WA SIMBA NA COASTAL UNION WASAKA VIPAJI


Timu ya Lusanga imeibuka Mabingwa Kombe la Mwanafa Cup baada ya kuichapa Ubembe FC  1 -0  huku Scout wa Simba SC na Coastal Union wakitinga kwenye fainali hizo  kujionea vipaji.

Mchezo  huo uliochezwa  Mei 26, 2024 katika Uwanja wa Jitegemee  Muheza umeshuhudiwa ukikusanya wapenzi na mashabiki wa soka, ambapo  Mbunge wa jimbo la Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, sanaa na michezo, mhe. Hamis Mwinjuma  amewaahidi wananchi wa Jimbo hilo  kuwa,  mwaka ujao mashindano hayo yatafanyika kwa ukubwa zaidi.

Timu ya Lusanga imejinyakulia Kombe na zawadi ya shilingi  milioni 5, Ubembe FC wamepokea shilingi milioni 3 kwa kwa kushika nafasi ya pili, mshindi wa tatu akipokea shilingi milioni 2 na mshindi wa nne amepokea milioni 1.

Aidha, mchezo huo umeshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani.

Jumla ya timu 133  katika vijiji vyote vya jimbo la Muheza vimeshiriki mashindano hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post