MBUNGE MAVUNDE KUWAWEZESHA KIUCHUMI WAJANE JIMBONI DODOMA MJINI


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameainisha mikakati ya kuwawezesha kiuchumi makundi maalum ya kwenye jamii likiwemo kundi la wajane ili kujikwamua kiuchumi.

Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wajane 250 wa Kata ya Nkuhungu Jijini Dodoma kwanye mkutano wa kusikiliza kero na changamoto zinazolikabili kundi hili.

“Tunaishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha tena mikopo ya 10% ambayo itachochea sana shughuli za kiuchumi na hasa kwa wakina mama.

Nimezungumza na Kampuni ya Sokoni Microfinance Ltd ambayo imefungua matawi yake hapa  Dodoma na wameonesha utayari wa kutoa mikopo kwa wajane bila riba hivyo nitahakikisha ninawasimamia vyema ili mnufaike na fursa hii na muondokane na mikopo ya kausha damu ambayo inawaachia madhara makubwa sana.

Sambamba na hiyo pia nitawaandalia mafunzo maalum ya ujasiriamali ili kuongeza ujuzi katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi “Alisema Mavunde

Akitoa salamu zake Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Bi. Asia Abdallah ameitaka jamii kutowatenga na kudhumu haki za wajane na kinyume chake iwaweke karibu na kusaidia utatuzi wa changamoto zao hasa za kiuchumi.

Akishukuru kwa niaba Mlezi wa Umoja wa Wajane-Nkuhungu Bi. Ashura Kimwaga amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kujali makundi yote katika jamii na kwamba wamejipanga kupitia umoja huu kuja na shughuli mbalimbali za kiuchumi za kuwainua wanawake ili kujiimarisha kiuchumi.

Post a Comment

Previous Post Next Post