MAPITIO USANIFU WA KUTOA MAJI MTO RUVUMA KWENDA MIKOA YA MTWARA NA LINDI KAZI IMEANZA


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso Bungeni Dodoma leo tarehe 03 April 2024 amesema Serikali tayari inafanya mapitio ya usanifu wa Mradi wa Kutoa Maji katika Mto Ruvu  kwenda kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.

Awali swali la msingi limeulizwa na Mhe Geoffrey Idelphonce Mwambe Mbunge wa Masasi Mjini 

alieuliza kuwa ni lini Serikali itakamilisha usanifu wa mradi wa maji ya Mto Rufiji yatokayo Bwawa la Julius Nyerere kupeleka Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo Waziri Aweso amejibu kwamba;

Serikali inaendelea na taratibu za tathmini ya awali ya usanifu wa mradi wa maji wa mto Rufiji kutoka katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere kupeleka kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la kuhakikisha inaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika mikoa hiyo. 

Aidha Waziri Aweso amesema kwasasa mpango unaoendelea ni kwamba tayari Serikali inafanya mapitio ya usanifu wa mradi wa kutoa Maji katika Mto Ruvuma kwenda kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi na maeneo ya pembezoni yatakayopitiwa na bomba kuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post