HATUSAJILI MAGROUP YA WHATSAAP


Serikali kupitia Msajili wa Jumuiya za  Kiraia imesema haisajili magroup ya WHATSAAP kama inavyoelezwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Akiongea na  waandishi wa habari leo Aprili 3, 2024 jijini Dar es Salaam, Msajili wa Jumuiya za Kiraia  Emmanuel Kihampa amesema katika maelezo yake aliyoyatoa kwenye mazungumzo yake ni kuwa kinachosajiliwa sio magroup ya  Whatsaap bali ni vikundi  vya Kiraia  ama taasisi za Kiraia ambavyo vimekuwa vinajiendesha kupitia magroup ya Whatsaap kutokana na ukuwaji wa Teknolojia hivyo vikundi ama asasi hizo hujikuta zinafanya mambo yao kama mikutano na majadiliano yao kupitia Magroup ya Whatsapp 

Kihampa amesema sababu ya kunukuliwa kusajili magroup ya Whatsaap ni kutokana na kuwa vikundi vingi vya Kiraia  vinajiendesha kupitia mtandao wa Whatsaap na kutokana na takwa la kisheria kuvitaka vikundi vyote vya kiraia ni lazima visajiliwe na sio magroup ya Whatsaap

Post a Comment

Previous Post Next Post