DK NCHIMBI AWAPATIA POLE WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO KAWETELE


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Nchimbi, pamoja na msafara wake, leo Jumatano, Aprili 17, 2024, amewatembelea kuwajulia hali na kuwapatia pole wananchi wa Kata ya Itezi, Wilaya ya Mbeya Mjini, walioathiriwa na maporomoko ya Mlima Kawetele, hivi karibuni. 

Mbali ya kuwasilisha salaam za pole za Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa waathirika hao wapatao 51, Dk Nchimbi, kwa niaba ya CCM, amewapatia pia pole ya fedha taslimu ya Sh. 10 milioni. 

Wananchi hao ambao wamepewa makazi ya muda Shule ya Msingi Tambuka Reli, Mbeya Mjini, walishukuru pole na salaam hizo za Chama na Serikali, huku Dk. Nchimbi akiwasihi kuwa na subira wakati huu ambapo Serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina juu ya tukio hilo ili kujua hatua stahiki za kuchukua kuzuia maafa zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post