AHADI YA RAIS SAMIA YATIMIA UJENZI BWAWA MONDULI


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (MB) amepokelewa kwa nderemo na Shangwe na Wananchi wa Vijiji cha Lepruko, Engaroji na Losimingori kufuatia ujenzi wa Bwawa la Lepruko ambalo ndio tegemeo kubwa kama chanzo cha Maji cha vijiji 3.

Ujenzi wa Bwawa hili ni ahadi ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan aliotoa kwa wana Monduli kata ya Lepruko walipokuja makao makuu ya serikali kuomba kujengewa Bwawa la kuhifandhi maji kutokana na changamoto kubwa ya ukosefu wa Maji Katika Kata hiyo tarehe 10 November 2023 na hivyo Rais Samia kuagiza Wizara ya Maji kutoa kiasi cha Tshs 532mil.

Aidha tarehe 11.11.2023 siku moja baada ya wananchi kupaza sauti Waziri Aweso alifika Lepruko wilayani Monduli mkoa wa Arusha kutoa ahadi kwa maelekezo ya Mhe Rais Samia ya kwamba kazi ya ujenzi wa Bwawa itatekelezeka ndani ya kipindi cha miezi sita pekee.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe Fred Lowasa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri amefika Kata Lepruko wilayani Monduli Mkoa wa Arusha na kushuhudia Bwawa hili likiwa limekamilika kwa 95% na tayari maji yameingia na kazi ya hatua ya mwisho inaendelea tayari kwa matumizi ya wananchi na mifugo.

Mwisho wananchi na Viongozi wa Kata ya Lepruko na wilaya ya Monduli kwa ujumla wamemshukuru kwa dhati Mhe Rais Samia kwa kuwajali na kutekeleza ahadi hii ndani ya miezi sita chini ya usimamizi thabiti wa Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso na Wizara ya Maji kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post