ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 92 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KILIMANJARO


Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa  zaidi ya shilingi Bilioni 92 kuboresha  huduma za afya  mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Mollel amebainisha hayo leo Machi 20, 2024  wakati akiwsalimia wananchi wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango aliyepo mkoani humo kwa ziara ya kikazi.

Dkt. Mollel amesema kuwa ndani kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza vifaa tiba kadha ikiwemo CT Scan kwenye  hospitali ya  KCMC, Mawenzi na Kibong'oto  zote  mkoani hapo.

Aidha amesema kuwa Rais Samia ametoa  shulingi bilion 7.9 katika hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro KCMC, ambapo shulingi bilioni  5.9 ni fedha za maendeleo, zaidi  ya shilingi bilion mbili za kuwezasha upatikanaji wa  vifaa tiba, dawa na vitendanishi.

“Serikali ya Dkt Samia  inalipa mishahara ya watumishi  wote  kwa asilimia 90 pale KCMC”, ameongeza Dkt. Mollel

Dkt. Mollel amefafanua kuwa, uwekezaji alioufanya Rais Samia katika sekta ya afya yeye na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu watahakikisha wanasimamia vema uwekezaji huo na kuleta tija kwa wananchi kupata Huduma bora za afya ili kuwa na taifa lenye ustawi.


Post a Comment

Previous Post Next Post