BILIONI 2 KUTUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa wa ndani pamoja na ujenzi wa uzio katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 210  kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ester Lukago Midimu aliyetaka kujua ni lini Serikali itajenga uzio katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu?

Dkt.Mollel amesema  kuwa  Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu ashaelekeza  Wizara kufanya  tathimini ya Madaktari bingwa  na Ubingwa bobezi  ili  kujua idadi  yao  katika  maeneo  waliopo  ili  kusambazwa  nchini  kulingana  na mahitaji  ya huduma  za ubingwa bobezi katika  mikoa

Post a Comment

Previous Post Next Post