SERIKARI KUFUNDISHA NA KUAJIRI WAHUDUMU NGAZI YA JAMII 137,294.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepanga kufundisha na kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 137,294 ndani ya miaka mitano, Ili kuhakisha kila mwanachi anafikiwa na huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa  Novemba 22, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitwaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt.Wilson Mahera wakati wa kikao kazi cha kupitia mtaala utakaotumika kufundishia wahudumu hao leo jijini Dodoma.

Dkt Mahera amesema kuwa lengo la serikali ni kuboresha huduma za afya nchini ili ziendane na uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya unaoendelea kwa kasi nchini.

‘’ Leo tumekusanyika hapa ili kupitia huu mtaala utakaotumika kuwafundishia wahudumu wetu,tunatarajia kuanza na wahudumu 28,000 mwaka 2024 na tutaendelea kadri tutakavyopata fedha.Tunategemea kuwa na wahudumu wawili katika  kila kitongoji kwa upande wa vijijini na mtaa kwa upande wa mijini na kila mhudumu atahudumia nyumba zisipungua 70”.

Dkt. Mahera ameongeza kuwa wahudumu hao watapewa mafunzo kwa muda wa miezi sita na kisha kuajiriwa rasmi na serikali. 

“Wahudumu hawa  baada ya kupata mafunzo ambayo yatakuwa ya nadharia na vitendo wataingizwa kwenye mfumo rasmi wa serikali na wataboreshewa maslahi yao ili waweze kufanya kazi kwa bidii.Wahudumu hawa watasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na upungufu wa wahudumu katika sekta ya afya nchini ili tufikie lile lengo la huduma ya afya kwa wote” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Ntuli Kapologwe, amesema kuwa wahudumu hao watajikita kwenye afua zaidi ya nane watakaosaidia kutambua magonjwa mapema ili wananchi wapate matibabu mapema.

“Pamoja na huduma za kitabibu,wahudumu hawa watatumika kutoa huduma za chanjo ,masuala ya lishe,ustawi wa jamii , kukabiliana na majanga kwenye ngazi ya jamii na kutoa elimu ya afya kwa umma.Mpango huu utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini na utakuwa wa mfano katika nchi zetu za Afrika.”

Programu hiyo ya kutoa mafunzo na kuajiri wahudumu hao inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 29.11.2023 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu

Post a Comment

Previous Post Next Post