WAZIRI .BITEKO AZITAKA WIZARA, TAASISI KUWA NA MIPANGO MAALUMU YA UENDELEZAJI MICHEZO MAHALI PA KAZI


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko amezitaka Wizara na Mashirika kuhakikisha yanakuwa na mpango maalumu wa kuendeleza michezo mahali pa kazi  ili kuleta tija na uwajibikaji kwa wafanyakazi. 

Biteko ameyasema hayo,  04 Oktoba 2023 Mkoani Iringa, wakati alipokuwa  akifungua rasmi michezo ya shirikisho la wafanyakazi kutoka Wizara na Idara za Serikali yanayoendelea Mkoani Iringa. 

Pia alisema ,Waajiri wanapaswa kutoa fursa kwa wafanyakazi kushiriki mashindano hayo kwani yana Lengo la kuwakutanisha Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi za Serikali ili kufahamiana. 

Nawaasa sana wanamichezo na Wafanyakazi mjiepushe na Rushwa na kuwa makini kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI na kuongeza ari ya kufanya kazi na uadilifu" Alisisitiza Biteko

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego alishukuru kwa michezo  ya SHIMIWI 2023 kufanyika Mkoani kwake, kwani  kumeleta hamasa na kusisimua mzunguko wa fedha na uchumi kwa ujumla kwenye mkoa huo. 

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa SHIMIWI Daniel Mwalusamba alisema kuwa mwaka huu kumekuwa na hamasa kubwa kwa waajiri kuleta idadi kubwa ya wanamichezo ambapo jumla ya Mikoa 25 ,wizara 24 ,na wakala 4,zimeshiriki  mashindano ya mwaka huu. 

Tunawashukuru waajiri Kwa kuendelea kuyapatia  kipaumbele mashindano haya kwa kutenga Bajeti za kutosha ili kufanikisha  ushiriki wa Watumishi katika michezo ya SHIMIWI.

Post a Comment

Previous Post Next Post