WATANZANIA WENGI ZAIDI KUWEZESHWA KIMITAJI KUSHIRIKI KATIKA UCHUMI WA MADINI


Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ametoa rai kwa Benki na Taasisi za fedha nchini kuiwesedha sekta binafsi na watanzania wengi zaidi kushiriki katika uchumi wa Madini na mnyororo mzima thamani kwenye sekta ya madini.

Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha pamoja katika ya Umoja wa Mabenki Tanzania(TBA) na wadau wa sekta ya madini kujadiliana namna bora ya sekta ya fedha inavyoweza kuchochea kukuza uchumi wa madini.

“Ni maelekezo ya Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaona watanzania wengi zaidi wanashiriki katika uchumi wa sekta ya madini.

Serikali imefanya marekebisho ya sheria na kutunga kanuni za kuwezesha ushiriki wa watanzania kwenye uchumi wa madini(Local content)

Niwaombe Taasisi za fedha mliopo hapa muwe sehemu ya uwezeshwaji wa kimtaki kwa watanzania kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma na uzalishaji wa bidhaa katika sekta ya madini.

Serikali itaendelea kuhakikisha inaweka mazingira bora zaidi ya ushiriki wa watanzania wengi katika uchumi wa madini”Alisema Mavunde

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania(TBA) Ndg. Theobald Sabi amesema Benki zipo tayari kuboresha ushirikiano mkubwa na sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wa sekta hii kwa kutoa mikopo ili kuwezesha mitaji ya shughuli za madini.

Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania(FEMATA) Ndg. John Bina ameishukuru Wizara ya Madini kwa hatua kubwa ya kuwakutanisha na wadau wa sekta ya fedha na kwamba hiyo ni hatua kubwa itakayopelekea kueleweka kwa sekta ya madini na kufanikisha kukopesheka kwa sekta.

Post a Comment

Previous Post Next Post