UKIKUTWA UNATUMIA VPN FAINI MILIONI TANO,KIFUNGO MWAKA MMOJA JELA


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi kwa ujumla na kampuni ambazo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya mtandao binafsi (VPN) hayazuiliki, kutoa taarifa TCRA juu ya VPN wanazotumia kabla ya Oktoba 30, mwaka huu.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kinyume cha kanuni.

Aidha, TCRA imesema itaendelea kudhibiti matumizi ya VPN yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa VPN ambazo hazijatolewa taarifa au kusajiliwa na kuongeza kuwa yeyote atakayebainika adhabu yake ni faini isiyopungua Tsh milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post