SERIKALI YA RAIS SAMIA INAENDELEA KUWEKEZA ILI KUPAMBANA NA UMASKINI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amesema kuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mageuzi makubwa yanayoendelea kufanyika nchini.

Waziri Prof. Kitila ametoa kauli hiyo leo October 16, 2023 katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mkoa wa Singida yaliyoambatana na mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Bombadia na kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Prof. Kitila ameeleza kuwa Serikali imewekeza katika Elimu, Afya, Maji, na miundombinu kwa kutumia fedha nyingi na kazi kubwa inafanyika kuhakikisha inapambana na umaskini

Jambo jingine la msingi linalofanywa na Serikali ni kuwezesha sekta za kiuchumi na ndio kazi kubwa inayofanywa, Mhe. Rais Kazi ambayo tuliahidi kupitia Chama cha Mapinduzi ya kupambana na umaskini inakwenda vizuri sana kupitia maeneo hayo" Amesema Waziri Prof. Kitila

Akisisitiza kwa kutumia maandiko ya Kwenye vitabu vya Dini Prof. Kitila amesema "Apandaye haba huvuna haba, Apandaye ukarimu huvuna ukarimu" na Rais Samia anapanda ukarimu kila pembe ya Nchi na hivyo atavuna ukarimu

Post a Comment

Previous Post Next Post