Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suhusu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya Kitaifa ya siku tatu Nchini Zambia, akiwa huko anatarajiwa kuhutubia Bunge tukufu la Nchi hio.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema Rais wetu wa Tanzania amepata heshima hiyo ambayo wameipata watu wachache kwenye nchi hiyo ya Zambia.
Waziri Makamba amesema >> 'Hii ni heshima kubwa na ya kipekee kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwani anakuwa mgeni mashuhuri wa nne kuhutubia Bunge hilo tangu mwaka 2012. Viongozi wengine waliowahi kuhutubia Bunge hilo ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki Moon mwaka 2012, Spika wa Baraza la Shirikisho la Urusi Mhe. Valentina Matvienko mwaka 2018 na Rais wa Italia Sergio Matarella 2022' - Waziri Makamba.
