Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Komredi Mussa Mwakitinya (MNEC) aingoza Viongozi mbalimbali wa UVCCM na wanachama kufanya usafi katika Nyumba Katibu wa UVCCM Mkoa Manyara leo Tarehe 09 Oktoba 2023.
Tukio hili ni muendelezo wa shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa ambapo Ndugu Mwakitinya alifanya uzinduzi Tarehe 08 Oktoba 2023 na kuanza kuongoza Shughuli za kijamii Katika Wilaya za Babati Vijijini na Hanang.
Akizungumza na Vijana mara baada ya Usafi katika Nyumba hio ya Mtumishi Komredi Mwakitinya amewaasa Vijana wa CCM kuwaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuyasema mambo mengi makubwa yanayofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Aidha Komredi Mwakitinya ameendelea kuwaasa Vijana mkoani Manyara kuwapuuza Wapinzani na wanaharakati ambao wao hawaoni kazi kubwa zinazofanywa na Serikali za CCM wao wamejikita katika upotoshaji na kudhihaki Viongozi wa Chama cha Mapinduzi.
"Kamwe tusikubali kupotoshwa na Wapinzani na wanaharakati ambao hawana kazi ya kufanya kazi yao ni kudhihaki na kujifanya Vipofu wa kazi kubwa zinazofanywa na Serikali za CCM katika Taifa letu". Alisema Mwakitinya
Mwisho Komredi Mwakitinya amewaalika Vijana kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kusherehekea wiki ya Vijana kitaifa na kilele cha Mbio za Mwenge Mkoani Manyara.
