Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe Nicholaus George Ngassa ameungana na Waumini wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora kufanya adhimisho la Misa Takatifu ya kumpongeza Mwadhama Protase Kadinali Rugambwa.
Misa Takatifu imefanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu lililopo Tabora Mjini. Misa imehudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Tabora, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Madhehebu ya Dini na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Tabora nà Majimbo mengine ya Ndani na Nje ya Nchi.
Tunamtakia matashi mema Mwadhama Protase Kadinali Rugambwa katika utumushi akiongozwa na Neno Takatifu "... Enendeni Ulimwenguni Kote (EUNTES IN MUNDUM UNIVERSUM).." MK 16: 15.
Tags
Habari
