Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejipanga kutoa fedha kwa wakimama kwa ajili ya kufanya utafiti wa kisayansi katika upande wa usalama wa chakula.
Akizungumza leo Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Vituo vya Ubunifu na Utafiti vilivyowezeshwa na COSTECH, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt. Beatrice Lyimo, amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha wanatarajia kutoa fedha kwa wakimama ili waweze kufanya utafiti.
Dkt. Lyimo amesema kuwa lengo ni kuendelea kutoa fedha kwa ajili wabunifu pamoja na watafiti ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa.
"Wanaume wengi wanapata fursa ya kukopa fedha na kufanya utafiti tofauti na wakimama" amesema Dkt. Lyimo.
Amebainisha kuwa asilimia 70 wanaume wamekuwa wakipata fursa ya kupata mkopo na kufanya utafiti.
Dkt.Dkt. Lyimo ameeleza kuwa bado hawajaaza kutoa fedha, huku akieleza kuwa watatumia njia mbalimbali ikiwemo mashindano ya kibunifu ili kuwapata wakinamama wabunifu.
