Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Komredi Mussa Mwakitinya (MNEC) amesema kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 Chama cha Mapinduzi hakina Mhombea Mwingine Zaidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassaan
"Kwa kazi kubwa anazozifanya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan sisi chama cha Mapinduzi kuelekea Uchaguzi mkuu 2025 hatuna mgombea Mwingine zaidi ya Mama Samia, tumeahuhudia kazi kubwa na Mapinduzi makubwa kwenye Sekta za kiuchumi, kijamii na kisaisa katika Taifa letu. Kwa maendeleo haya tunaamini atashinda kwa kishindo 2025" Alisema Mwakitinya.
Ndugu Mwakitinya ameyasema hayo wakati anazungumza na Vijana Mkoa wa Manyara katika Nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara tarehe 09 Oktoba 2023.
Tags
Siasa
