Tanzania na Canada zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya utafiti wa kina wa madini, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiolojia, kuhamasisha uwekezaji na kuendeleza Sekta ya Madini nchini.
Hayo yameelezwa Juni 16,2026. Wakati wa kikao cha Waziri wa Kilimo Mhe Anthony Mavunde na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Emily Burns, kilicholenga kujadili namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika eneo la utafiti wa madini.
Tanzania hivi sasa inajipanga kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na badala yake kuwa na uchimbaji unaoongozwa na taarifa muhimu za kijiolojia,huku akisisitiza kuwa mkakati uliopo ni kuongeza eneo lililofanyiwa utafiti wa kina kutoka asilimia 16 ya sasa hadi asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.
Tanzania na Canada zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na kwamba ameridhishwa na dhamira iliyooneshwa na Serikali ya Canada ya kushirikiana na Tanzania katika miradi ya kimkakati ya utafiti wa kina wa madini.
Kwa upande wake, Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Emily Burns, amesema Serikali ya Canada imevutiwa na maono ya *Mining Vision 2030* pamoja na kaulimbiu ya *“Madini ni Maisha na Utajiri”*, na kueleza kuwa nchi hiyo ipo tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo utafiti wa kina wa madini kwa kutumia teknolojia ya uchunguzi wa angani kupitia ndege maalum.
