MBUNGE MAHAWANGA JANETH AZINDUA KIKUNDI CHA WANAWAKE WAJANE KATA YA KIJICHI WILAYA YA TEMEKE


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth ameungana na kuzindua Umoja wa Wanawake Wajane (UWANE) Kata ya Kijichi Wilaya ya Temekewanaojihusisha na ujasiriamali wa kilimo cha mboga mboga na biashara ndogo ndogo.

Mh. Mahawanga amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono juhudu za Wanawake wajasiriamali nchini na kuhakikisha anaendelea kutafuta fursa mbalimbali zinazoendelea kustawisha uchumi wa Wanawake katika shughuli zao mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Mh. Mahawanga ameendelea kuwahamasisha Wanawake wa makundi yote kuhakikisha wanajiunga vikundi, wanasajili na kufanya shughuli za ujasiriamali kwa pamoja ili waweze kuchangamkia fursa za mikopo isiyo na riba lakini pia kuwa na miradi ya pamoja itakayowatengenezea  ajira na kulinda mitaji yao.

Mh. Mahawanga amewataka Wanawake wajasiriamali wote wa kikundi cha Wajane kuhakikisha wanakuwa na malengo ya kuinuana kiuchumi, kudumisha upendo baina yao, kutiana moyo lakini pia kuendelea kuwapokea wenzao ambao bado hawajajiunga kwani kuna kundi kubwa sana la Wanawake Wajane ambao bado wanajitafuta.

Lakini pia Mh. Mahawanga amewapongeza Wajasiriamali hao kwa kufanya usajiri wa umoja wao, na amewakubalia ombi lao la kuwa mlezi wao na kuwahaidi hatawaacha katika safari yao badala yake atahakikisha wanatimiza ndoto na malengo yao waliyojiwekea yanatimia.

Mhe. Mahawanga amewasihi sana Wanawake wa Umoja wa Wajane kutumia vizuri muungano wao kwa kuhakikisha wanajiandikisha na wanashiriki kikamilifu kwenye zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mtaa, vile vile Wanawake wenye sifa muda utakapofika wakachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo kwani yeye anaamini Wanawake ni viongozi wazuri na waaminifu sana.

Mwisho Mh. Mahawanga ametoa wito kwa Wanawake wa kikundi cha Wajane kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kwani yeye yupo pamoja nao katika kila hali na lengo lake kubwa ni kuona uchumi wa Wanawake wa Dar es Salaam unaimarika kwani shughuli kubwa naya msingi kwa Wanawake wa Dar ni biashara, na Dar es Salaam ni jiji na lango la biashara hivyo amewataka kuitumia vizuri fursa hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post